1 Chronicles 11:10-41

Mashujaa Wa Daudi

(2 Samweli 23:8-39)

10 aHawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi. 11 bHii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

12Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 13 cHuyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. 14 dLakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

15 eWakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 16 fWakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. 17Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” 18 gKwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 19Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

20 hAbishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 21 iAlitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

22 jBenaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 23 kAlimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano.
Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.
Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao.
24Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 25Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

26 mWale watu mashujaa walikuwa:
Asaheli nduguye Yoabu,
Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
27 nShamothi Mharori,
Helesi Mpeloni,
28 oIra mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa,
Abiezeri kutoka Anathothi,
29 pSibekai Mhushathi,
Ilai Mwahohi,
30Maharai Mnetofathi,
Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,
31 qItai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini,
Benaya Mpirathoni,
32Hurai kutoka mabonde ya Gaashi,
Abieli Mwaribathi,
33Azmawethi Mbaharumi,
Eliaba Mshaalboni,
34wana wa Hashemu Mgiloni,
Yonathani mwana wa Shagee Mharari,
35Ahiamu mwana wa Sakari Mharari,
Elifale mwana wa Uru,
36Heferi Mmekerathi,
Ahiya Mpeloni,
37Hezro Mkarmeli,
Naarai mwana wa Ezbai,
38Yoeli nduguye Nathani,
Mibhari mwana wa Hagri,
39Seleki Mwamoni,
Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
40 rIra Mwithiri,
Garebu Mwithiri,
41 sUria Mhiti,
Zabadi mwana wa Alai,
Copyright information for SwhNEN